1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Paul Kagame

Paul Kagame ndiye rais wa sita na wa sasa wa Rwanda, akiwa madarakani tangu mwaka 2000, wakati mtangulizi wake Pasteur Bizimungu alipojiuzulu. Kagame aliongoza kikosi cha waasi kilichokomesha mauaji ya kimbari 1994.

Kagame alizaliwa katika familia ya Kitusti kusini mwa Rwanda Oktoba 23, 1957. Alipokuwa na miaka miwili, mapinduzi ya Rwanda yalihitimisha udhibiti wa kisiasa wa Watusti uliyodumu kwa karne kadhaa, familia yake ilikimbilia nchini Uganda alikoishi utoto wake wote. Katika miaka ya 1980 Kagame alipigana katika jeshi la uasi la Yoweri Museveni, na kuwa afisa wa juu wa jeshi baada ya ushindi wa kijeshi wa Museveni kumpeleka madarakani. Kagame alijiunga na kundi la "Rwandan Patriotic Front" RPF, lililoivamia Rwanda mwaka 1990, kiongozi wake Fred Rwigyema aliuawa mapema katika vita na Kagame akachukuwa uongozi. Kufikia mwaka 1993, RPF ilikuwa inadhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Rwanda na makubaliano ya kusitisha mapigano yakasainiwa. Mauaji ya rais wa Rwanda Juvenal Habyariman yalisababisha mauaji ya kimbari ambamo watu 800,000 waliuawa. Kagame alianzisha tena vita vilivyokomesha mauaji hayo na kuishia kwenye ushindi wa kijeshi. Amebadilisha katiba na kumruhusu kuendelea kutawala baada ya kumaliza muhula wake wa sasa mwaka 2017, na huenda akaitawala nchi hiyo hadi mwaka 2034.

Onesha makala zaidi