Polisi Ujerumani wavamia nyumba za washukiwa wa itikadi kali | Habari za Ulimwengu | DW | 24.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi Ujerumani wavamia nyumba za washukiwa wa itikadi kali

-

BERLIN

Polisi nchini Ujerumani wamefanya misako katika nyumba kadhaa na maofisi ya watu wanaoshukiwa kuwa ni wanaharakati wa siasa kali za kiislamu kama sehemu mojawapo ya uchunguzi dhidi ya watu hao.Polisi katika jimbo la kusini la Bavaria wametoa taarifa ikisema kwamba uvamizi huo ulifanywa katika nyumba 16 kote nchini ujerumani ikiwa ni pamoja na katika miji ya Bonn na Berlin.Polisi wamekusanya stakabadhi chungunzima kwa ajili ya uchunguzi.Aidha polisi imesema kuwa watu tisa wengi wakiwa ni wa asili ya kigeni wanatuhumiwa kujaribu kushawishi na kuwatia moyo watu kufuata siasa kali za kidini na kuwataka kuunga mkono shughuli za kuendesha vita vya Jihad nchini na nje ya nchi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com