Pato la ndani lapungua Ujerumani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 15.05.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Pato la ndani lapungua Ujerumani

Pato la ndani lashuka kwa asilimia 3.8 nchini Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Katika robo ya kwanza ya mwaka huu pato la ndani lilinywea kwa asilimia 3.8 nchini Ujerumani.

Idara kuu ya takwimu imetoa taarifa hiyo leo mjini Berlin inayoonesha kwamba Ujerumani ,hakika imo katika kina kirefu cha mdodoro wa uchumi kisichokuwa na kifani tokea kumalizika vita kuu ya pili.Uchumi wa Ujerumani ulirudi nyuma katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Idara kuu ya takwimu ya serikali ya mjini Wiesbaden imearifu kwamba pato la ndani ya nchi lilinywea kwa asilimia 3.8 katika kipindi hicho.Wataalamu wa uchumi wamesema Ujerumani haijawahi kukabiliwa na mserereko wa uchumi wa kiwango hicho tokea kumalizika vita kuu vya pili.

Hii ni kwa mara ya nne mfululizo kwamba pato la taifa limenywea nchini Ujerumani. Kupungua kwa pato la taifa kunafuatia kunywea kwa uchumi wa nchi kwa asilimia 2.2 katika robo ya mwisho ya mwaka jana.Wataalamu wa uchumi wamesema hawakutarajia mserereko huo mkubwa.

Hatahivyo uchumi wa Ujerumani ulionesha dalili za kuanza kutengemaa mnamo mwezi wa aprili. • Tarehe 15.05.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HrLS
 • Tarehe 15.05.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HrLS
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com