PARIS:Segolene Royal kufanya mjadala wa televisheni na Francois Bayrou | Habari za Ulimwengu | DW | 28.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS:Segolene Royal kufanya mjadala wa televisheni na Francois Bayrou

Mgombea wa Urais nchini Ufaransa Segolene Royal na mpinzani wake aliyeshindwa Francois Bayrou wanakutana leo kwenye mjadala wa Televisheni kufuatia mvutano juu ya sheria za uchaguzi.

Nicolas Sarkozy ambaye atapamabana kwenye duru ya pili na Royal hapo mwezi Mei 6 amekataa kushiriki mjadala huo akisema atajadiliana juu ya suala hilo na bibi Royal Pekee.

Francois Bayrou amemshutumu Sarkozy kwa kuzuia mazungumzo huru.

Kitu muhimu kinachosubiriwa ni kuona nani atapata kura milioni 6.8 za bwana Bayrou katika uchaguzi wa duru ya pili ingawa hadi sasa bwana Bayrou hajamuunga mkono mgombea yoyote kati ya Sarkozy na bibi Royal.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com