Operesheni ya kiutu, bunge la Ujerumani laidhinisha jeshi la majini kujiunga na jeshi la umoja wa Ulaya katika pembe ya Afrika. | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Operesheni ya kiutu, bunge la Ujerumani laidhinisha jeshi la majini kujiunga na jeshi la umoja wa Ulaya katika pembe ya Afrika.

Bunge la Ujerumani limeidhinisha jeshi lake la majini kujiunga na jeshi la umoja wa Ulaya katika kupambana na maharamia katika eneo la pembe ya Afrika.

Maharamia wakitweka karibu na meli ya kifahari ya Marekani M/s Nautica katika juhudi za kuiteka nyara meli hiyo katika pwani ya Yemen katika eneo la ghuba ya Aden.

Maharamia wakitweka karibu na meli ya kifahari ya Marekani M/s Nautica katika juhudi za kuiteka nyara meli hiyo katika pwani ya Yemen katika eneo la ghuba ya Aden.


Bunge la Ujerumani , Bundestag leo Ijumaa limeidhinisha ushiriki wa jeshi la majini la nchi hiyo katika ujumbe wa umoja wa Ulaya unaojulikana kama Atalanta ikiwa ni juhudi za kuimarisha ulinzi katika eneo la maji la pembe ya Afrika.

Katika eneo hilo jeshi hilo litakuwa na kazi ya kuzuwia maharamia kuteka nyara meli , na kusababisha njia hiyo ya kibiashara majini kuwa katika hatari. Chini ya sheria za kimataifa ,jukumu la jeshi hilo, ambalo litakuwa na kiasi cha wanajeshi 1,400 wa Ujerumani, linatokana na azimio la umoja wa mataifa.


Meli za kivita katika operesheni hiyo ya Atalanta, zinapaswa kuwasaka na kupambana na maharamia, ndivyo inavyoelezwa katika rasimu ambayo ilipitishwa kwa wingi mkubwa katika bunge la Ujerumani, Bundestag. Umuhimu kwa serikali ya Ujerumani ni ulinzi wa meli za mpango wa chakula duniani ambazo zinapeleka misaada ya chakula nchini Somalia. Zaidi ya Wasomali milioni tatu wanategemea misaada hii, anasema Rolf Mützenich kutoka chama cha SPD.


Ndio sababu ni muhimu, kwa meli hizi zinazobeba bidhaa kupewa ulinzi. Kwamba maisha ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa ni muhimu kabisa. Kwa hiyo ushiriki wa jeshi la majini la Ujerumani ni operesheni ya kiutu.Lakini pia ni operesheni inayotilia maanani maslahi ya meli za kibiashara , na hususan ni muhimu kwa bidhaa zinazosafirishwa nje za Ujerumani. Ujerumani imeamua kutuma meli yake ya kivita ya Karlsruhe, yenye helikopta mbili ndani. Kuwapo kwa takriban meli sita za kijeshi kutoka bara la ulaya , serikali ya Ujerumani inataraji kuwa kutawatisha maharamia wa Kisomali kutoka katika pwani ya nchi hiyo. Mwanasiasa kutoka chama cha CDU Ruprecht Polenz ameonya hata hivyo kuwa na matarajio makubwa.

Tunazungumzia eneo la karibu kilometa za mraba milioni tatu. Hii ni mara nane ya ukubwa wa Ujerumani. Nani anamini kuwa sasa kila tukio la utekaji nyara la maharamia linaweza kuzuiwa, na kama hiyo haitawezekana , kutofanikiwa kwa operesheni Atalanta, mtu anayefikiria hivyo anaweka kiwango cha juu mno ambacho , utaratibu wa kiusalama hauwezi kuvukwa.


Kwa mtazamo wa chama cha mrengo wa shoto cha Linke kuwapo kwa meli za kivita hakuleti chochote. Maharamia wataendelea kufanya uhalifu wao pale ambapo meli ya kivita haipo, amesema Paul Schäfer, kwa hiyo serikali inaweza kubadili kauli yake hapo baadaye.

Najiuliza, tunapata wapi imani hii, kwamba operesheni hii kubwa itamaliza uharamia? Meli za kivita 11, ziko tayari katika eneo hilo, ambazo tunazizungumzia. Katika muda wa saa 48 meli nne zimetekwa nyara. Kwa nini tunakuwa na uhakika hivyo.


Serikali ya Ujerumani hata hivyo haina haja ya kuwakamata maharamia, na kwa hiyo kuna suali lenye utata la m kisheria , wapi na vipi watu hao wanaweza kufikishwa mahakani. Vyama vyote lakini vinakubaliana kuwa , sababu za uharamia nchini Somalia zinakutikana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na kutokuwapo mfumo wa kiutawala. Pia , iwapo kuna ugumu wa nchi hiyo kuisaidia , ni lazima kutafuta njia za kuisaidia.

►◄
 • Tarehe 19.12.2008
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GJq8
 • Tarehe 19.12.2008
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GJq8
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com