Nuri al Maliki asema ratiba ya kuondoka majeshi ya Marekani iwekwe | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.07.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Nuri al Maliki asema ratiba ya kuondoka majeshi ya Marekani iwekwe

Je pendekezo hilo la Iraq linakubaliwa na rais Bush?

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki

Kwa mara ya kwanza waziri mkuu wa Iraq Nouri al Maliki ametamka wazi hadharani kwamba nchi yake inataka paweko ratiba ya kuondoka nchini Iraq wanajeshi wa Marekani pamoja na suala hilo kujumuishwa katika mazungumzo yanayoendelea na serikali ya mjini Washington.

Waziri mkuu huyo wa Iraq hakutoa maelezo zaidi juu ya suala hilo lakini mshauri wa masuala ya kiusalama wa taifa amefahamisha kuwa serikali imeandaa mapendekezo ya kutaka itolewe ratiba ya wanajeshi hao wa Marekani kuondoka Iraq itakayotokana na uwezo wa vikosi vya Iraq wa kuweka hali ya usalama nchini humo.

Hata hivyo mjini Washington wizara ya mambo ya nje imekataa kutoa tamko lolote kuhusiana na kuendelea mazungumzo kama hayo na Iraq.

Rais Goerge W Bush anapinga vikali pendekezo hilo.

 • Tarehe 08.07.2008
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EY38
 • Tarehe 08.07.2008
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EY38
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com