NURENBERG: Ujerumani yakubali kutoa vibali vya kuishi nchini Ujerumani wakimbizi laki nne | Habari za Ulimwengu | DW | 17.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NURENBERG: Ujerumani yakubali kutoa vibali vya kuishi nchini Ujerumani wakimbizi laki nne

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka majimbo 16 yanayounda muungano wa Ujerumani wanaokutana mjini Nuremberg, wamefikia maridhiano juu ya mpango wa serikali ya muungano ya kuwapatia wageni kiasi ya 200,000 vibali vya kuishi nchini Ujerumani.

Wageni hao ambao ni wakimbizi waliomba hifadhi nchini Ujerumani wakakataliwa ila hawakurudishwa nyuma. Chini ya makubaliano hayo, 20,000 ambao tayari wana kazi wataruhusiwa kuomba kibali cha kuishi nchini Ujerumani bila kupoteza muda.

Wengine 40,000 watapewa muda wa kufikia mwezi Septemba mwaka ujao wawe wamepata kazi kabla ya kuweza kuomba kibali cha kuishi nchini Ujerumani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com