NEW YORK: Umoja wa mataifa wailaumu Eritrea kuingia katika eneo la usalama kati yake na Ethiopia | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Umoja wa mataifa wailaumu Eritrea kuingia katika eneo la usalama kati yake na Ethiopia

Umoja wa mataifa umeituhumu nchi ya Eritrea kuwapeleka wanajeshi na vifaru vya kijeshi katika eneo la usalama lililowekwa kati ya nchi hiyo na Ethiopia. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, ameitaka Eritrea iwaondowe wanajeshi wake kutoka eneo hilo la usalama ili kuepuka kuhatarisha mkataba wa kukomesha mapigano uliofikiwa miaka 6 iliopita. Wanajeshi wa Umoja wa mataifa wanashika doria kulichunguza eneo la kilomita 1000 lililotengwa na Umoja wa mataifa kati ya nchi hizo mbili katika juhudi za kuvimaliza vita vya miaka miwili ambavyo vilisababisha mauaji ya watu zaidi ya 70,000.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com