NEW YORK: Feruji yakwamisha shughuli katika sehemu ya New York- Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 16.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Feruji yakwamisha shughuli katika sehemu ya New York- Marekani

Zaidi ya watu 320,000 hawana umeme na shughuli zimekwama katika jimbo la New York nchini Marekani kufuatia feruji nyingi ilioanguka katika eneo la kando kando ya kiunga cha Buffalo.

Feruji hiyo ambayo imefikia sentimeta 60 kutoka ardhi, ilikuwa nyingi kuwahi kutokea kwa muda wa miaka 140 iliopita na wataalamu wa hali ya hewa wanahofia kutokea mafuriko makubwa wakati feruji hiyo itakapotoweka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com