NEW DEHLI: Watu 12 wauawa katika ajali ya treni magharibi mwa India | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DEHLI: Watu 12 wauawa katika ajali ya treni magharibi mwa India

Kwa uchache watu 12 wameuawa na wengine kiasi ya 50 wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu ndani ya treni ya abiria katika jimbo la Bengal, magharibi mwa India. Mripuko umesambaratisha treni hiyo karibu na kijiji cha Belakova na polisi wanahofia huenda kukawa na watu ambao bado wamenasa katika mabaki ya kipande cha treni kilichopasuka. Hadi sasa haijajulikana ni nani amehusika na shambulio hilo. Hata hivyo, polisi wanayashukia makundi ya wanaharakati wanaotaka mjitengo magharibi mwa majimbo ya Bengal na Assam. Hilo ndilo lilikuwa shambulio la bomu baya zaidi tangu mwaka 1999 ambapo wanajeshi 10 wa serikali ya India waliuawa katika shambulio la bomu lililovizia treni iliokuwa ikiwapeleka kwenye uwanja wa mapigano katika eneo la Kashmir linalogombaniwa na India na Pakistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com