Mwanasoka bora wa AFRIKA | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 31.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Mwanasoka bora wa AFRIKA

CAF inachagua leo mwanasoka wa mwaka wa Afrika mjini Lome.

Baada ya duru ya kwanza ya Kombe la Afrika la mataifa kukamilika jana na washindi wanajiwinda kwa duru ijayo ya robo-finali mwishoni mwa wiki hii ,macho yanakodolewa leo nchini Togo,jirani na Ghana.Afrika inachagua huko „mwanasoka bora wa mwaka“ na usoni kabisa katika orodha hiyo ni nahodha wa Ivory Coast-Didier Drogba,Michael Essien wa Ghana na Frederic Kanoute wa Mali.

Beki mashuhuri wa Ivory Coast na Arsenal,Kolo Toure,pengine asichezea mpambano ujao wa robo-finali na Guinea.

Na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani inarudi uwanjani leo kwa mpambano kati ya viongozi wa Ligi-Bayern Munich na Hansa Rostock.

Nahodha wa Corte d’Iviore Didier Drogba anakabiliwa leo na changamoto kali kutoka kwa mwenzake wa Chelsea-Michael Essien wa Ghana na stadi wa Mali, Frederic Kanoute katika kinyan’ganyiro cha kuania taji la mchezaji bora wa dimba wa mwaka wa Afrika.

Magoli ya drogba yaliiweka chelsea kilelelni mwa msimu uliopita kunyan’ganyia taji la premier League-Ligi ya uingereza na alichangia mno kwa Chelsea kulibaka kombe la FA.Ni yeye alietia bao pekee dhidi ya Manchester United uwanjani Wembley.

Stadi mwenzake wa Chelsea-Michael Essien aliemaliza nafasi ya 3 mara 2 katika kinyan’ganyiro kilichopita cha taji hili,pia alitamba na Chelsea pamoja na Drogba.Lakini kutocheza sana kwa Ghana mwaka jana ,kunaweza kukamnyima tena Essien taji hilo.

Frederic Kanoute wa Mali anaeichezea Sivilla –klabu yake ya Spian,aliteuliwa katika orodha hii kwa mchango wake uliopelekea Mali kushiriki katika kombe hili la Afrika la mataifa nchini Ghana.Nafasi za ushindi leo kwa kanoute zinanawirishwa zaidi na kuisaidia Sevilla kushinda kombe la ulaya la UEFA na lile la nyumbani Spain la King’s cup.

Ikiwa Kanoute atashinda, itakua kwa mara ya kwanza kwa mzaliwa wa Ulaya kuvaa taji hilo la Afrika .Kwani, Frederic Kanoute aliwahi kuichezea timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa kabla hakuamua kuichezea Mali –nchi yake ya asili hapo 2004.

Zawadi hii ya leo inaamuliwa na makocha 53 wa Afrika .

Wakati wa kufanya sherehe hii mjini Lome, Togo-jirani na Ghana,umekosolewa na Essien amekataliwa ruhusa kwenda Lome wakati Kanoute ni ruhusa kuhudhuria .Ghana ina miadi na mahasimu wao wa jadi Nigeria jumapili hii wakati nahodha wa Ivory Coast, Drogba ataongoza hujuma za Corte d’Iviore dhidi ya Guinea mjini Sekondi siku hiyi hiyo.Mali ilipigwa kumbo nje ya mashindano haya jumaane wiki hii.

Hapa Ujerumani, baada ya likizo ya x-masi na mwaka mpya, Bundesliga-Ligi ya Ujerumani inarudi uwanjani leo kwa changamoto kati ya viongozi wa ligi-Bayern Munich na Hansa Rostock.Munich itacheza na kocha wake wa zamani Ottmar Hitzfeld kabla kocha mpya Jürgen Klinsmann kuchukua usukani msimu mpya ukianza majira ya kiangazi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com