Mtuhumiwa wa mauaji ya 1994 ya Rwanda akamatwa ufaransa | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 10.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Mtuhumiwa wa mauaji ya 1994 ya Rwanda akamatwa ufaransa

---

PARIS

Polisi nchini Ufaransa imemkamata afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda Marcel Bivugabagabo ambaye anatafutwa na mahakama ya Rwanda kubabiliana na kesi ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Afisa huyo wa zamani jeshini mwenye umri wa miaka 53 aliyekamatwa jumatatu ni miongoni mwa watu waliorodheshwa katika majina ya wahalifu wa kivita wanaosakwa na serikali ya mjini Kigali.Marcel huenda akarudishwa Rwanda wakati wowote.Marcel lakini hayumo kwenye orodha ya majina ya wahalifu wanaotakiwa na mahakama ya kimataifa ya mjini Arusha Tanzania inayoshughulikia kesi ya mauaji ya Rwanda.

Kamanda huyo wa zamani wa kundi la Ruhengeri anadaiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ambapo watu laki nane wengi watutsi waliuwawa nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com