Mshukiwa ugaidi amekamatwa nchini Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mshukiwa ugaidi amekamatwa nchini Ujerumani

KARSLRUHE:

Raia wa Ujerumani alie na asili ya Kipakistan amekamatwa na polisi kusini-magharibi ya Ujerumani akishukiwa kulisaidia kundi la kigaidi la Al-Qaeda.Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu,mshukiwa huyo alifanya safari mara nne katika eneo la mpaka wa Afghanistan na Pakistan kati ya mwezi Aprili mwaka 2005 na Juni 2007.Kila safari,aliwapa wanamgambo wa Al-Qaeda pesa zisizopungua Euro 4,000.Mshukiwa huyo mwenye miaka 45 anashutumiwa pia kuingiza kimagendo vifaa vya redio na darubini kwa kundi la Al-Qaeda na kuhudhuria mafunzo ya kutumia mabomu kwenye kambi moja nchini Pakistan.

Ujerumani,kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani,ilipitisha sheria inayoruhusu kuwafunga jela wanachama wa makundi ya kigeni ya kigaidi hadi miaka 10.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com