Moscow. Vyama vinavyounga mkono serikali vyashinda uchaguzi.
12 Machi 2007Matangazo
Matokeo ya mwanzo katika uchaguzi wa majimbo yameviweka vyama viwili vinavyounga mkono serikali mjini Moscow katika nafasi ya uongozi.
Chama cha United Russia, kinachoungwa mkono na rais Vladimir Putin , kinatarajiwa kuthibitishwa kushinda, wakati chama cha Fair Russia kimeonyesha uwezo mkubwa. Mashirika ya habari yanasema kuwa vyama hivyo viwili vimepata kati ya asilimia 50 na 70 ya kura.