MOSCOW: Ndege ya shehena yanguka nchini Urusi
29 Julai 2007Matangazo
Ndege ya shehena aina ya Antonov,imeanguka muda mfupi tu baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo mjini Moscow.Maafisa wamesema,watu wote 8 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamefariki.Sababu ya ajali kwa hivi sasa,bado haijulikani.Ajali hiyo imetokea saa chache tu baada ya helikopta moja kuanguka katika eneo la Udmurtiya kwenye milima ya Ural ya Urusi.Kwa mujibu wa maafisa,helikopta hiyo iligusa kebu za umeme kabla ya kuanguka kwenye bwawa.