MOSCOW: Marekani yatuhumiwa kuchochea mashindano ya silaha | Habari za Ulimwengu | DW | 01.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Marekani yatuhumiwa kuchochea mashindano ya silaha

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema,majeribio ya makombora yaliyofanywa na nchi hiyo siku ya Jumatano ni jibu la moja kwa moja kwa mipango ya Marekani ya kutaka kuweka makombora ya ulinzi katika Jamhuri ya Czech na nchini Poland. Alipozungumza na waandishi wa habari mjini Moscow,Putin aliishutumu Marekani kuwa inaanzisha upya mashindano ya silaha.Akasema,Urusi itaendelea kuimarisha silaha zake ili uwepo usawa wa nguvu duniani.Rais Putin ametamka hayo juma moja kabla ya kukutana na rais wa Marekani George W.Bush na viongozi wengine katika mkutano wa madola manane yaliyoendelea kiviwanda duniani G-8 utakaofanyawa mji wa Heiligendamm,nchini Ujerumani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com