Mkutano wa Amani na Usalama mjini Kampala,Uganda
5 Oktoba 2009Matangazo
Akizungumza wakati wa ufunguzi,
wa mkutano wa amani na usalama mjini Kampala, Rais Museveni aliwatolea
wito waafrika waamke na wapiganie maslahi yao na si kunyamaza kimya
kwani kimya chao ni ishara ya uoga na hakuna amani inayoweza kupatikana
kama upande mmoja unanung'unika kimya kimya.
Mwandishi wetu kutoka Kampala Leyla Ndinda, alihudhuria mkutano huo na ametuandalia taarifa ifuatayo.
Mwandishi: Leyla Ndinda
Mpitiaji :Munira Muhammad