1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa Lisbon bado wakumbwa na upinzani

21 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/ENoy

BRUSSSELS

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekiri kwamba jamhuri ya Czech huenda ikashindwa kuudhinisha mkataba wa Lisbon ambao tayari umeshakataliwa na wapiga kura wa Ireland.

Hata hivyo baada ya kikao chao mjini Brussels hapo jana viongozi hao wamesema shughuli ya kuudhinisha mkataba huo katika jamhuri ya Czech imesimamishwa kutokana na matatizo ya kisheria lakini itaendelea katika nchi zingine za Umoja huo.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameonya dhidi ya kuchukuliwa muda mrefu wa kuutafakari mkataba huo kwasababu tayari imeshachukua miaka miwli kuutayarisha mkataba huo mpya baada ya kukataliwa kwa katiba ya Umoja wa ulaya na nchi za Ufaransa na Uholanzi mwaka 2005.

Viongozi wa Umoja wa ulaya wameahirisha hadi mwezi wa Oktoba uamuzi juu ya namna ya kulishughulikia tatizo la Ireland la kuukataa mkataba wa Lisbon katika kura ya maoni wiki iliyopita na wakati huohuo wakitafuta njia za kuondokana na pingamizi ya jamhuri ya Czech kuelekea mkataba huo.