1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz asema Ujerumani haitoshiriki vita dhidi ya Iran

19 Machi 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema kuwa hakuna mpango wa kushawishi unaoonesha kuwa operesheni ya Marekani na Israel dhidi ya Iran itafanikiwa.

https://p.dw.com/p/5Af39
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Nico Herbertz/IMAGO

Merz ameyasema haya katika hotuba yake mbele ya bunge la Ujerumani, Bundestag. Katika hotuba hiyo, Merz amesema Ujerumani haikushauriwa na Marekani kabla kuanza kwa vita hivyo kwani ingepinga kufanyika kwa operesheni hiyo.

Kansela huyo vile vile amedai kuwa Ujerumani haitoshirikikwa njia ya kijeshi kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz. Kauli ya Kansela Merz imekuja baada ya waziri wake wa ulinzi Boris Pistorius Jumatatu kusema Ujerumani haikuvianzisha vita hivyo kwa hivyo haitojihusisha.

Viongozi wa Ulaya wamekataa kuhusishwa moja kwa mojakatika operesheni za Israel na Marekani dhidi ya Iran, wakihofia kuzamishwa ndani ya mzozo usiotabirika na ambao malengo yake hayako wazi na mzozo ambao raia wa mataifa ya Ulaya hawauungi mkono.