Maziwa kutoka China marufuku nchini Burundi na Tanzania | Masuala ya Jamii | DW | 23.09.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Maziwa kutoka China marufuku nchini Burundi na Tanzania

Kashfa ya maziwa yaliyokuwa na sumu aina ya melamine imechukua mkondo mpya baada ya watoto yapata alfu 53 kutangazwa kuathiriwa nchini Uchina.

default

Mtoto aliyeathirika na maziwa yaliyokuwa na sumu huko China

Kwa sasa mkaguzi mkuu wa usalama wa chakula nchini humo tayari amefutwa kazi kufuatia taarifa hizo.Jumla ya watoto wanne wanaripotiwa kufariki jambo lililopelekea baadhi ya mataifa kupiga marufuku uingizaji na usambaaji wa maziwa na bidhaa za maziwa kutoka Uchina.Mataifa hayo yanajumuisha Bangladesh,Brunei,Japan,Malaysia,Myanmar,Singapore,Burundi na Tanzania.Kemikali ya melamine hutumika kutengezea bidhaa za plastiki na husababisha athari za figo katika mwili wa binadamu.

Ili kupata ufafanuzi wa hatua hiyo nchini Tanzania Thelma Mwadzaya amezungumza na Gaudencia Simwaza afisa wa uhusiano katika Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa.
Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com