Mawaziri wa fedha wa G20 wakubaliana kuimarisha uchumi. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.11.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mawaziri wa fedha wa G20 wakubaliana kuimarisha uchumi.

Mawaziri wa fedha wa mataifa ya G20 wamekubaliana kuendelea na mpango wa serikali kuimarisha uchumi wa mataifa yao.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble, kushoto, waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner, kati, na waziri wa fedha wa Uingereza Alistair wakati wa mkutano huo wa G20 mjini St. Andrews, Scotland.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble, kushoto, waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner, kati, na waziri wa fedha wa Uingereza Alistair wakati wa mkutano huo wa G20 mjini St. Andrews, Scotland.

Mawaziri wa Fedha kutoka nchi za kundi la G-20 wamekubaliana kuendelea na mpango wa serikali kuimarisha uchumi wakihofia kuongezeka kwa idadi ya wakosa ajira na nakisi ya bajeti. Katika mkutano wao mjini St.Andrews huko Scotland, mawaziri hao vile vile wameafikiana kuhusu ratiba ya mfumo mpya wa kusimamia uchumi wa nchi zao.

Lakini hakuna makubaliano yaliyopatikana kuhusu njia ya kusimamia gharama za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble akijitokeza kwa mara ya kwanza katika jukwaa la kimataifa tangu kushika wadhifa wake huo mpya amessema kuwa amesikitishwa na matokeo hayo.

Kwa upande mwingine, wajumbe wa mashirika makuu ya misaada na haki za binadamu katika mkutano wao mjini Berlin, wametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kila kiwezekanacho ili kuhakikisha kuwa mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa utakaofanywa mjini Copenhagen mwezi wa Desemba utafanikiwa.

 • Tarehe 08.11.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KQpE
 • Tarehe 08.11.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KQpE
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com