Marekani yapewa mwezi mmoja kuokoa mazungumzo ya amani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Marekani yapewa mwezi mmoja kuokoa mazungumzo ya amani

Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wataipa Marekani muda wa mwezi mmoja kuyaokoa majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati yaliyokwama.

Palestinian President Mahmoud Abbas, left, Arab League Secretary General Amr Moussa, center and Egyptian foreign minister Ahmed Aboul Gheit arrive to attend an Arab foreign ministers meeting at the Arab league headquarters in Cairo, Egypt Thursday, July 29, 2010. The Palestinian president is refusing to move to direct peace negotiations with Israel, as the Arab League meets Thursday to decide whether to add its weight to U.S. and Israeli pressure for face-to-face talks. (AP Photo/Nasser Nasser)

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu,Amr Moussa(kulia) pamoja na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas(kushoto).

Mawaziri hao wa mambo ya nje waliokutana katika mji wa Sirte nchini Libya wamesema, uamuzi huo umepitishwa ili kuzuia kuvunjika kwa majadiliano ya ana kwa ana yaliyoanzishwa upya kati ya Waisraeli na Wapalestina, mwanzoni mwa mwezi wa Septemba.

Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas alisitisha majadiliano hayo baada ya Israel kukataa kurefusha muda wa kusitisha ujenzi wa makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi.Muda huo ulimalizika mwisho wa mwezi wa Septemba.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com