1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine

14 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema msaada wa kijeshi wa Marekani uko njiani kuelekea Ukraine na utaleta tofauti kubwa katika uwanja wa mapambano.

https://p.dw.com/p/4fqaR
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Blinken atembelea Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, kushoto, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, kulia, kabla ya mkutano wao huko Kyiv, Ukraine, Jumanne, Mei 14, 2024.Picha: Brendan Smialowski/AP/picture alliance

Akifafanua zaidi waziri huyo alisema "Tunafahamu hiki ni kipindi kigumu lakini pia tunajuwa hivi karibuni msaada uko njiani. Sehemu ya msaada umeshawasili. Na mwingine zaidi utawasili na utaleta tofauti kubwa katika kukabiliana na uchokozi unaoendelea wa Urusi katika uwanja wa mapambano. Na tumejidhatiti pamoja na washirika wengine wengi wa Ukraine kuhakikisha kwamba mnafanikiwa katika uwanja wa mapambano. Halikadhalika tumedhatiti kwa muda kuona Ukraine inasimama imara kivyake.'' Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za Juu wa Marekani aliyeko katika ziara ambayo haikutangazwa mjini Kiev amefanyamazungumzo na rais Volodymyr Zelensky ambaye ameomba nchi yake ipatiwe mifumo zaidi ya ulinzi kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya Urusi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Urusi imekamata eneo la ukubwa wa takriban kilomita 125 za mraba ambalo linajumuisha vijiji vipatavyo saba kwa mujibu wa taarifa ya vyanzo vinavyofuatilia matukio katika eneo hilo.Ziara ya Blinken imelenga kumpa uhakika mshirika wake Ukraine katika vita hivyo vya Urusi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW