Maoni ya wahariri wa magazeti. | Magazetini | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri wa magazeti.

Katika maoni yao,wahariri wa magazeti leo wanazungumzia juu ya uamuzi wa serikali ya Ujerumani kupeleka ndege za doria aina ya Tornado nchini Afghanistan.

Gazeti la NORDKURIER juu ya uamuzi wa serikali ya Ujerumani kulepeka ndege za doria aina ya Tornado nchini Afghanistan linasema kuwa kwa muda wa miezi kadhaa Kansela wa Ujerumani alikuwa anapinga wazo hilo.

Na hata kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za NATO uliofanyika mjini Riga kansela Angela Merkel alikataa ombi la katibu mkuu wa jumuiya hiyo pamoja na la rais Bush wa Marekani juu ya askari wa Ujerumani kusaidia kusini mwa Afghanistan.

Naye mhariri wa gazeti la WIESBADENER KURIER katika maoni yake anauliza ni kwa muda gani Ujerumani itaendelea kujiweka kando na mapambano nchini Afghanistan wakati sasa inapeleka ndege zitakazotumika kwa ajili ya kukusanya habari muhimu, ili kuyawezesha majeshi kufanya mashambulio? Mhariri anasema kuwa majeshi ya Ujerumani pia yatakuwamo mstari wa mbele wa mapigano kuanzia mwezi wa aprili ikiwa bunge litaidhinisha uamuzi huo wa kulepeka ndege za kivita.

Hivyo hivyo basi anasema mhariri wa gazeti la FRÄNKISCHEN kuwa siyo kweli kusema kuwa ndege hizo hazitashiriki katika mapambano. Mhariri huyo anaeleza kwamba marubani wa ndege hizo watalazimika kushambulia ikiwa watatishiwa na makombora. Anaejaribu kukataa ukweli huo anaepa wajibu wake, pia kwa watu wa Afghanistan.

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linaeleza matumaini kwamba ndege za Ujerumanai zitashiriki katika mapambano dhidi ya ugaidi kwa kiwango kadirifu.

Mhariri wa gazetia la BADISCHE TAGBLATT anasema yapasa kutilia maanani kwamba Ujerumani ina askari 2900 nchini Afghanistan, ambao ni sehemu ya jeshi la kimataifa linalopambana na matilaban japo baadhi ya watu nchini Ujerumani hawataki kuona hivyo.

Mhariri huyo anasisitiza kuwa maadui wa jeshi hilo la kimataifa ni matalibani, na hivyo basi ni wajibu wa nchi za magharibi kuleta demokrasi na kujenga utengemavu nchini Afghanistan ili kuiepusha nchi hiyo kujerejea tena katika utawala wa waislamu wenye siasa kali.