Maoni ya wahariri wa magazeti | Magazetini | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri wa magazeti

Jopo la wataalamu wa uchumi nchini Ujerumani limeitahadharisha serikali ya Kansela Merkel dhidi ya kurudi nyuma katika utekelazaji wa sera za maguezi . Wahariri wa magazeti leo wanazingatia tahadhari hiyo katika maoni yao.

Katika ripoti yao ya mwaka juu ya uchumi wa nchi wataalamu hao wameishauri serikali ya kansela Merkel, asilani isirudi nyuma katika kutekeleza mageuzi muhimu , la sivyo mafanikio yaliyofikiwa katika miaka ya hivi karibuni yatahatarishwa.

Juu ya ripoti ya wataalamu hao mhariri wa gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG anasema hali iliyopo sasa nchini Ujerumani ni nzuri lakini serikali ya mseto ya Kansela Merkel haitumii fursa hiyo vizuri kwa sababu haina mpango unaoeleweka.

Mhariri huyo pia anakumbusha ushauri wa wataalamu wengine wa uchumi waliosema siku nyingi kuwa ustawi wa uchumi nchini Ujerumani umetokana na mageuzi yanayotekelezwa sasa.

Na kutokana na hayo,serikali ya bibi Merkel achane kabisa na wazo la kurudi kisengere nyuma katika utekelezaji wa mageuzi hasa katika sekta ya pensheni na posho kwa ajili ya watu wasiokuwa na ajira.

Mhariri anasema anatumai alieanzisha mjadala juu ya kufanya mabadiliko katika sehemu fulani za sera za mageuzi - mwenyekiti wa chama cha SPD bwana Kurt Beck amesikia vizuri yanayosemwa na wataalamu hao.

Gazeti la ROSTOCKER OSTSEE linaunga mkono hoja ya mhariri wa ALLGEMEINE ZEITUNG kwa kusema ustawi wa uchumi ni sawa na nyendo za hali ya hewa- mara baridi mara joto !

Kwa kusema hyayo mhariri wa gazeti hilo anamaanisha kwamba ni maamuzi ya viongozi yanayoathiri michakato ya uchumi.

Mhariri huyo anasema anaetumia kwa busara, fursa nzuri iliyopo sasa nchini, huyo hana haja ya kuwa na wasiwasi juu ya siku za usoni.

Gazeti la ROSTOCKER OSTSEE linasema, kuwa ni wazo la kufurahisha sana kurefusha muda wa kutoa posho kwa wazee wasiokuwa na ajira. Pia ni wazo la kuchangamsha juu ya kubadilisha uamuzi kuhusu kustaafu na umri wa miaka 67.

Lakini mhairiri anasisitiza kuwa hapana budi kuzingatia ushauri wa wataalamu wa uchumi wanaosema ,huu siyo wakati wa kuchezea mafanikio yaliyofikiwa katika kutekeleza sera za mageuzi.

Na mhariri wa gazeti la MAIN ECHO anasema serikali ya mseto ya Kansela Merkel inagueza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa kuwa dau la kuchezea kamari.

AM.