Mamia kwa Maelfu ya Wakristo wameshiriki katika maandamano ya Ijumaa kuu mjini Jerusalem. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 21.03.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mamia kwa Maelfu ya Wakristo wameshiriki katika maandamano ya Ijumaa kuu mjini Jerusalem.

Mamia kwa maelfu ya mahujaji wa Kikristo kutoka duniani kote wameanza maandamano mjini Jerusalemu.

Viwanja vya Mtakatifu Petro, vikionyesha Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Viwanja vya Mtakatifu Petro, vikionyesha Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

katika eneo la mji mkongwe leo Ijumaa kupitia katika njia aliyopitia Yesu Kristo wakati akisulumbiwa tukio ambalo ndiyo linakumbukwa hii leo.

Waamini, wengi wao wakiwa wamevaa misalaba wameonekana wamejazana katika Mtakaa wa Via Dolorosa au njia ya mateso ambayo Yesu anasemekana kuwa aliipitia akiburuza msalaba ambao baadaye alisulubiwa juu yake na warumi.

Njia hiyo inaanzia nje ya nyumba ya watawa ambapo Yesu alipigwa, kukejeliwa, na kuvishwa taji la miba.

Wawakilishi kutoka familia mbili za Waislamu ambao wamekuwa wakihifadhi funguo za Kanisa lililojengwa mahali alipofia Yesu Kristo tangu karne ya kumi na tatu walifungua milango ya Kanisa hilo kwa ajili ya Waamini.

Jeshi la Polisi liliongezewa nguvu ili kuzuia tukio lolote la hatari ambalo linaweza kujitokeza wakati wa maadhimisho hayo.

Israel imeiunganisha Jerusalemu ya Mashariki ikiwa ni pamoja na mji mkongwe baada ya Vita vya Mashaariki ya Kati vywa mwaka 1967 na kuutangaza mji huo kuwa hautagawanyika kamwe.

Dai hilo la Taifa la Uyahudi halitambuliwi na jumuiya ya Kimataifa.

Akizungumzia kuhusu siku ya Ijumaa Kuu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri nchini Tanzania Alex Gehaz Malasusa, alielezea kuhusu hali ilivyo katika siku hii ya maombolezo kwa Wakristo nchini humo.

Askofu Mkuu Malasusa amesema tangu jana Wakristo wameonekana wakifurika katika makanisa yao na kwamba hali hiyo inaonyesha mwamko zaidi wa kiimani.

Akitoa ujumbe kuhusu siku hii kwa nchi za eneo la Maziwa makuu Askofu Malasusa amesema ni vema wakristu wakatambua kwamba Kristu alikufa msalabani ili watu wote wakombolewe.

Amesema katika kipindi cha kwaresma kila mtu anapaswa kujitafakari na nakuwasaidia wenye mahitaji kwa kuzingatia matatizo mbalimbali yaliyoko kwenye jamii.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Injili ya Wakristo, inaonyesha kwamba katika siku ya tatu baada ya Yesu kusulubiwa alifufuka. Tukio hilo linaadhimishwa kama siku ya Pasaka, ikiwa ni siku muhimu sana kwa Wakristo.

 • Tarehe 21.03.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DSPh
 • Tarehe 21.03.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DSPh
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com