Mahojiano na Seif Shariff Hamad wa Zanzibar akiwa ziarani Ulaya
19 Februari 2010Matangazo
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar limepitisha kwa kauli moja kuyakubali na kuyaimarisha maridhiano yaliofikiwa na rais wa nchi hiyo, Amani Karume, na katibu mkuu wa Chama kikuu cha upinzani cha CUF nchini Tanzania, Maalim Seif Shariff Hamad. Baraza limetaka uitishwe Visiwani humo kura ya maoni kuwauuliza wananchi kama wanawafiki kuundwa serekali ya umoja wa kitaifa kutokana na vyama vinavowakilishwa kwenye Baraza hilo. Hivi karibu Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa ziarani Italy na Uingereza, Othman Miraji alizungumza naye kwa njia ya simu. Alitaka kwanza kujua chama chake cha CUF kinafikiria juu ya hatua gani za kikatiba na kisheria zipitwe ili kufikia lengo hilo:
Mhariri:Thelma Mwadzaya