Mahojiano na Professa Issa Shivji, kuhusiana na uteuzi wa Dokta Billal.
12 Julai 2010Matangazo
Rais Jakaya Kikwete pia jana alimtangaza rasmi Dokta Gharib Billal kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi huo wa Oktoba.
Uteuzi huo wa Dk Bilal, CCM, umekuja baada ya halmashauri kuu ya chama hicho kumchagua Dokta Ali Mohammed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na kumuacha Dokta Bilal ambaye pia alikuwa akiwania nafasi hiyo, pamoja na wagombea wengine na kuzua malalamiko kutoka kwa wafuasi wake.
Hivi punde Halima Nyanza alizungumza na Profesa Issa Shivji, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania kutaka kujua hatua hiyo ya kuchaguliwa Dokta Bilal kuwa mgombea Mwenza wa rais Kikwete inaashiria nini?