Mageuzi ya kifedha nchini Marekani yanaendelea lakini kuna upinzani mkubwa kutoka kwa wadau. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mageuzi ya kifedha nchini Marekani yanaendelea lakini kuna upinzani mkubwa kutoka kwa wadau.

Ulikuwa mradi mkubwa wa rais wa Marekani Barack Obama wa mageuzi ya kifedha.

default

Rais Barack Obama sera zake za mageuzi ya kifedha zinapingwa vikali na makundi yenye ushawishi mkubwa .

Ulikuwa mradi mkubwa sana wa rais wa Marekani Barack Obama , mradi huo mkubwa wa mageuzi ya kifedha katika muda wa miaka 80, ulipaswa kuziweka benki kuu za Marekani katika mstari, kudhibiti ulanguzi na kuwalinda mateja katika hali bora zaidi. Na hususan ulipaswa kuzuwia mizozo mingine ya hapo baadaye ya kifedha. Lakini upinzani wa mabenki dhidi ya sheria kali ni mkubwa, na unagharamiwa kwa kiwango kikubwa.

Kileleni mwa eneo la kibiashara mjini New York wanapatikana wanaume na wanawake 150 na ndio wanaoendesha mambo ya fedha. Ukumbi wa mauzo wa benki ya Mellon unaonekana kama kituo cha watu wanaotafuta kibarua. Benki hiyo inamilikiwa na watu hawa, ambao katika wiki zilizopita walituma kikosi chao ili kuweza kupenyeza ushawishi wao mjini Washington.

mabenki makubwa yanawekeza kwa pamoja zaidi ya dola milioni moja, ili kuweza kuleta ushawishi katika siasa, ili wanasiasa wawatambue. Wanayohaki hiyo, anasema Michael Woolfolk, mkuu wa kitengo cha mikakati cha benki hiyo ya Mellon.

Kuwapa fedha wale wanaofanya ushawishi ni sehemu ya kawaida ya utamaduni wa kisiasa. Ni wasemaji, watetezi wa shughuli za fedha, ambao wameathirika. Kwa hiyo mabenki haya ambayo yanaathirika na sheria hiyo yana watetezi wao, ambao wanajaribu kulinda maslahi ya wenye hisa katika mabenki hayo.

Superbowl , ni tamasha kubwa kabisa la kimichezo duniani, pamoja na michezo linashughulikia aina mbali mbali ya sherehe kwa ajili ya maslahi ya matukio ya michezo. Wale wanaoendesha ushawishi wanatambua, linaandika gazeti la Time na wamekwisha toa fedha. Rais Obama amesema wakati wa mkutano wa G20 kuwa benki zitapaswa kugharamia matatizo yao wakati wa mizozo, zinapaswa kuanzisha mfuko wao , lakini haukuweza kuanzishwa. Lakini hilo si suala pekee ambalo rais Obama anapaswa kulitambua. Kwa mfano ulanguzi, serikali yake inataka , kuachana na ulanguzi wa mali zenye hatari kwa makampuni tanzu. Wazo hilo , kwamba fedha za wateja wa kawaida zitatengwa kando na kuangaliwa na dola ambazo zinaongia katika ulanguzi wa hatari. Benki zinadai kuwa , haziwezi kuondokana na ulanguzi. Ndio sababu kwa karne kadha zimeweza kupata uhakika wa faida. Lakini mtu anaweza pia kufanya biashara ya kubahatisha na kisha akapoteza kila kitu. Kwa gharama ya baadaye pamoja na marekebisho ya bei, ama hata pia kufilisika kwa mataifa. Michael Woolfolk analiangalia tatizo hilo.

Sasa unaingia katika ulanguzi wenye utata zaidi, na kisha unaingia katika hali ya kuvutia zaidi kuanzia hapo. Baadhi ya nyakati ulanguzi unakuwa na utata sana ambapo mtendaji wa soko ambaye ananunua ama kuuza mali hizi hafahamu kwa undani hatari iliyopo. Kufanya biashara ya ulanguzi katika nchi nyingine, hii itaongeza gharama.

Katika mpango wa kutenganisha na shughuli zote za kibiashara sheria hizi mpya zitakuwa zimegusa sehemu ndogo tu ya ulanguzi. Madai ya kawaida yanayofahamika yatakuwa yameshughulikiwa , kwa kuweka mipaka ya kitaifa ya kiutaratibu.

Mwandishi :Steffens Frauke/ZR/Kitojo Sekione

Mhariri:Abdul-Rahman Mohammed

E N D E

 • Tarehe 12.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OHZW
 • Tarehe 12.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OHZW
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com