Maafisa 16 wa polisi wauwawa na Taliban nchini Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Maafisa 16 wa polisi wauwawa na Taliban nchini Afghanistan

Wanamgambo wa Taliban wamekishambulia kituo cha polisi kusini mwa Afghanistan na kuwaua maafisa 16 wa polisi.

Msemaji wa wizara ya ndani ya Afghanistan amesema leo kwamba maafisa hao walikuwa wakishika doria katika kituo hicho katika wilaya ya Maywand mkoani Kandahar.

Msemaji wa Taliban, Zabiullah Mujahid, amethibitisha kwamba kundi hilo limefanya maujai hayo. Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ya Afghanistan imetangaza kwamba wanajeshi wanne wameuwawa kwenye mlipuko wa bomu katika mkoa wa Uruzgan.

Mwanajeshi mwingine mmoja ameuwawa kwenye mlipuko mwingine uliotokea katika mkoa wa Paktia.

Maafisa wawili wa polisi pia wameuwawa leo wakati gari lao lilipolipuliwa na bomu mkoani Helmand.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com