LUSAKA. Rais Mwanawasa atarajiwa kushinda uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 02.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA. Rais Mwanawasa atarajiwa kushinda uchaguzi

Tume ya uchaguzi nchini Zambia imesema , rais wa sasa Levy Mwanawasa anatarajiwa kushinda uchaguzi baada ya matokeo ya majimbo 135 kati ya majimbo 150 kutangazwa. Mpinzani wa rais Mwanawasa Michael Sata amekubali kushindwa huku matokeo kamili yakisubiriwa kutangazwa na tume ya uchaguzi.

Sata amesema kutokana na rais Levy Mwanawasa kuongoza kwa wingi mkubwa ni shida kuziba pengo hilo. Pamoja na hayo mgombea huyo wa chama cha Patriotic Front amesema mizengwe iliyofanyika imeshampa Mwanawasa zaidi ya kura milioni moja. Akizungumza na radio DW mpiga kura mmoja kutoka mjini Lusaka ameeleza msimamo wa matokeo ulivyo hadi sasa kama ilivyo tangazwa na tume ya uchaguzi nchini Zambia.

O Ton…taarifa za hivi punde zilmesema hadi sasa bwana Mwanawasa amepata asilimia 43 ya kura Michael Sata asilimia 27.7 na Hakainde Hichileama wa chama cha United Democtaric Alliance asilimia 26.98.

Bwana Sata amewataka wafuasi wake kuwa watulivu. Awali wafuasi wa rais Levy Mwanawasa na wale wa mpinzani wake Michael Sata walikabiliana na polisi baada ya kuzusha ghasia huku vurugu za uchaguzi zikizagaa hadi katika maeneo manne ya mji wa Lusaka yanayokaliwa na watu wenye hali duni.

Polisi walilazimika kufyatua risasi hewani kuwazuia watu waliotaka kupora mali kutoka madukani katika eneo la Garden na pia walitumia gesi ya kutoa machozi katika mitaa ya Mandevu, Chipata na Bauleni kwa ajili ya kutawanya makundi ya watu yanayo ongezeka huku hali ya wasiwasi ikitanda kabla ya matokeo kamili kutangazwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com