LONDON: Rais Yusuf yuko tayari kukutana na wapiganaji wa Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Rais Yusuf yuko tayari kukutana na wapiganaji wa Somalia

Rais wa Somalia, Abdulahi Yusuf Ahmed, amesema yuko tayari kukutana na wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo wa wastani katika juhudi ya kuzuia damu kuendelea kumwagika nchini humo.

Akizungumza akiwa ziarani mjini London Uingereza, rais Yusuf, alisema kundi lolote linalotaka kufanya mazungumzo sharti kwanza liweke silaha chini na liachane na machafuko.

Aidha kiongozi huyo alisema serikali ya mpito ya Somalia inadhibiti maeneo yote ya nchi lakini kudumisha usalama, sheria na utengamano itachukua muda.

Mapema wiki hii watu takriban 12 waliuwawa mjini Mogadishu kwenye mapigano mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia walipowafurusha wanamgambo wa mahakama za kiislamu mwishoni mwa mwaka jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com