Ligi ya Ujerumani. | Michezo | DW | 03.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ligi ya Ujerumani.

Luiz Gustavo ajiunga na Bayern Munich kutoka Hoffenheim.

default

Luiz Gustavo uwanjani.

Katika uhamisho wa kuufungua mwaka 2011, Bayern Munich inaamini kujiimarisha kikosi chake sasa baada ya kufanikiwa kujinyakulia mchezaji wa kiungo cha kati, Luiz Gustavo, kutoka Hoffeinheim.

Makubaliano ya kumnunua Mbrazil huyo yalifikiwa mnamo wikendi hii iliyokwisha baada ya mwekezaji mkuu ,wa timu ya Hoffeinheim, Dietmar Hopp, kuidhinisha uuzaji huo.

Na kabla ya Hoffeinheim kuhimili pengo hilo, Mkufunzi Ralf Rangnick amejiuzulu kufuatia uhamisho wa Gustavo ambao alikuwa akiupinga tangu awali.

DFB-Pokal 1899 Hoffenheim - Borussia Mönchengladbach

Kocha Ralf Rangnick.

Kocha huyo, mwenye umri wa miaka 52, ameeeleza kwamba hatua ya kuuzwa Gustavo iliiashiria wazi kwake kwamba timu hiyo haihitaji kocha kama yeye,na lililomshangaza zaidi ni kugundua kwamba mazungumzo ya uhamisho wa Gustav yalianza mwezi uliopita pasi yeye kujuwa.

Kocha Rangnick amekuwa akijipanga kwa mashindano ya kufuzu ya Ligi ya Europa lakini mwekezaji huyo mkuu wa Hoffeinheim amekuwa makini kujaribu kujinufaisha kifedha kwa takriban Euro milioni 150 zilizolipwa kumnunuwa Gustav.

Vyombo vya habari Ujerumani vinasema kwamba Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, Bayern imekubali kumnunuwa kwa kiasi hicho cha fedha,baada ya hapo awali kununuliwa na Hoffeinheim kwa Euro milioni moja kutoka Corinthias Alagoano.

Kabla ya kuanza mapumziko ya msimu wa baridi, Hoffeinheim ilikuwa katika nafasi ya nane katika Bundesliga na wamo katika robo fainali ya mashindano ya komba la Ujerumani DFB.

Kwa waliofaidi, inaonekana sio mwisho kwani kocha wa Bayern Munich Louis van Gaal ameashiria kwamba huenda timu hiyo ikamsajili mshambuliaji wiki hii.

Tusubiri tuyaone, kwa sasa Gustavo ameajiunga rasmi na timu yake mpya ya Bayern iliopo mjini Qatar kwa mazoezi na anatarajiwa kuonyesha umahiri wake wa kusakata soka kwa uwezo wake wa kucheza kiungo cha kati  na ulinzi kikiwemo kiungo cha beki kushoto.

Sio mchezo rafiki yangu!

Mwandishi:Maryam Abdalla/Dpae

Mhariri:Othman Miraji