Kundi la MEND lasema halikuhusika na mauaji Nigeria | Matukio ya Afrika | DW | 03.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Kundi la MEND lasema halikuhusika na mauaji Nigeria

Maafisa wa polisi ya Nigeria wanaendelea kuwasaka washukiwa waliohusika na shambulio hilo la bomu

Wapiganaji wa Kundi kubwa zaidi nchini Nigeria, MEND, wamekanusha madai kwamba walihusika katika shambulio lililotokea mwishoni mwa wiki lililowauwa watu wanne mjini Abuja. Polisi bado wanaendelea kuwasaka wahalifu waliohusika kwenye shambulio hilo. Awali, kundi la MEND linalodai kuwa linayatetea maslahi ya jamii zinazoishi kwenye Bonde la Delta la mafuta mengi lilikiri kuhusika katika shambulio jengine lililowauwa watu 12 mwezi wa Oktoba. Kulingana na taarifa ya kundi hilo, wapiganaji wake hutoa ilani kabla ya kulivamia eneo lolote ili kuzuwia maafa kutokea.

Shambulio la Ijumaa lilisababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine 26. Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililojitokeza kukiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea wiki moja baada ya mapigano yaliyo na misingi ya kidini kusababisha maafa mjini Jos.