Kiev. Uchaguzi wa mapema waahirishwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kiev. Uchaguzi wa mapema waahirishwa.

Rais wa Ukraine Viktor Yushchenko ameahirisha uchaguzi wa mapema kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja na kuweka tarehe 24 Juni kuwa siku ya uchaguzi huo.

Akizungumza katika hotuba kwa taifa hilo, Yushchenko amesema anapanga kutumia wakati huu kujaribu kutatua mzozo wake wa kisiasa na waziri mkuu Viktor Yanukovich.

Serikali yake imekataa kutii amri ya rais inayotaka kufanyika uchaguzi na mapema, ikisema kuwa hatua hiyo inakwenda kinyume na katiba.

Yanukovich ametumia wingi katika bunge kuzuwia fedha kwa ajili ya uchaguzi huo.

Suala hili hivi sasa linaangaliwa na mahakama ya kikatiba ya Ukraine.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com