Khartoum. Majeshi kutoka nje ya Afrika hayahitajiki, asema Konare. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Khartoum. Majeshi kutoka nje ya Afrika hayahitajiki, asema Konare.

Mwenyekiti wa umoja wa Afrika , Alpha Oumar Konare , amesema kuwa majeshi ambayo sio ya kutoka katika mataifa ya Afrika hayatahitajika kuwa sehemu ya jeshi la pamoja kati ya umoja wa Afrika na umoja wa mataifa litakalowekwa katika jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

Katika taarifa kufuatia mkutano wake na rais wa Sudan Omar al-Bashir mjini Khartoum , Konare amesema amepata ahadi za kutosha za uchangiaji wa majeshi kutoka mataifa ya Afrika. Serikali ya Sudan inapinga majeshi kutoka nje ya bara la Afrika kushiriki katika jeshi hilo la pamoja , ambalo litaundwa na wanajeshi 20,000 wa kulinda amani na maafisa 6,000 wa polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com