1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani ameridhika na sera za serikali yake ya mseto

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUGY

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesisitiza mafanikio ya serikali yake ya mseto katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.Katika hotuba yake mbele ya bunge la Ujerumani mjini Berlin, Merkel alisema sera za kiuchumi za serikali yake zimesaidia kupunguza idadi ya wakosa ajira kwa milioni moja tangu mwaka 2005.Akasisitiza kuwa serikali yake ya mseto itaendelea kufuata njia hiyo ya mageuzi na uwekezaji.