Kampuni ya Ujerumani yatuhumiwa kuhusika na rushwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.07.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ujerumani

Kampuni ya Ujerumani yatuhumiwa kuhusika na rushwa

Kampuni inayohusika na programu za kompyuta ya nchini Ujerumani yahusishwa na madai ya rushwa. Kwa miaka kadhaa shughuli za biashara za familia ya Gupta ya huko nchini Afrika Kusini zimekuwa zikijadiliwa kikla uchao

Kampuni inayohusika na programu za kompyuta ya nchini Ujerumani yahusishwa na madai ya rushwa. Kwa miaka kadhaa shughuli za biashara za familia ya Gupta ya huko nchini Afrika Kusini zimekuwa zikijadiliwa. Waandishi wa habari hivi sasa wanatuhumu, kuwa watengenezaji wa programu za kompyuta kutoka Ujerumani ambao ni kampuni ya SAP walilipa hongo kwa kampuni hiyo ya familia ya Gupta. Zainab Aziz anatusomea ripoti ya mwandishi wa DW Martina Schwikowski.

Familia ya Gupta yenye ushawishi mkubwa ni familia ya wafanyabiashara kutoka India na  inalaumiwa kwa kuitia mikononi Afrika Kusini kwa sababu ndugu watatu wa familia hiyo ni marafiki wa karibu wa Rais Jacob Zuma. Katika mikataba mbalimbali familia hiyo imekuwa na usemi mkubwa hata katika ugawaji wa na nafasi kwenye baraza la mawaziri, pia katika mikataba ya biashara familia hiyo ilikuwa inapendelewa sana lakini kwa masikilizano kuwa ukoo wa rais Jacob Zuma utafaidika. Na mara hii kampuni inayohusika na programu za kompyuta ya nchini Ujerumani SAP ambayo ina tawi kubwa mjini Capetown, inatuhumiwa kushiriki katika vitendo vya rushwa.

Südafrika | Präsident Jacob Zuma (REUTERS/S. Hisham)

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na shirika la waandishi wa habari huru kiasi cha Euro milioni saba ziliwekezwa katika kampuni ya familia hiyo ya Gupta inayoishi nchini Afrika Kusini. Waandishi wa habari wanashuku kuwa kampuni ya Ujerumani ya SAP ilipata mkataba wa biashara baada ya kutoa hongo kwa familia hiyo ya Gupta ili kuweza kupata zabuni ya kufanya biashara na kampuni ya taifa ya Transnet huko Afrika Kusini.

Taarifa za barua pepe zilizopatikana ni mwanzo wa tu wa lelemama hiyo, kwa sababu mambo zaidi yanatarajiwa kufufuliwa. Siku ya Jumatatu waandishi hao wa habari walichapisha taarifa mpya inayoihusu kampuni hiyo ya Ujerumani na kuituhumu juu ya kushiriki katika vitendo vya rushwa kati yake na kampuni ya familia ya Gupta ili kudhibiti mkataba wa biashara. Kiasi cha fedha kinachotuhumiwa ni Euro milioni 12.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SAP Adaire Fox-Martin amesafiri kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuchunguza madai hayo kwamba kampuni yake imehusika na njia zisizo halali kwa ajili ya kupata mikataba yenye faida kubwa kutoka kwenye kampuni ya taifa ya usafiri ya Transnet.  Kampuni ya Transnet inasimamia shughuli za reli, bandari na mabomba ya kusafirishia mafuta. Kampuni ya Ujerumani ya SAP inasambaza programu za komputa kwa ajili ya usimamizi na udhibiti kwenye uwekezaji katika shughuli hizo. Ujerumani inaongoza katika soko la dunia, ina maelfu ya wateja duniani kote na inamiliki moja ya mifumo ya kisasa zaidi katika sekta ya teknolojia ya kuhifadhi taarifa.

Mnamo mwezi Machi mwaka 2016 wanachama wa chama kikubwa cha upinzani nchini Afrika Kusini walianzisha mjadala bungeni juu ya uhusiano kati ya familia ya Gupta na serikali ya rais Jacob Zuma.

Mwandishi:Zainab Aziz/Martina Schwikowsk/dw.com/p/2hGlB

Mhariri:Josephat Charo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com