KAMPALA : Uganda yatangaza hali ya hatari kwa mafuriko
21 Septemba 2007Matangazo
Uganda imetangaza hali ya hatari kufuatia mafuriko makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 30 katika eneo zima la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.
Takriban watu 270 wamekufa kutokana na mafuriko na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu katika nchi 18 zilizoathirika na mafuriko hayo.Umoja wa Mataifa na Chama cha Msalaba Mwekundu vimetowa wito wa msaada wa fedha kusaidia watu milioni moja walioathirika na mafuriko hayo.
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema imeongeza msaada wake kwa wahanga wa mafuriko Afrika kwa uero 430,000.