KABUL:Kambi ya jeshi la Ujerumani yashambuliwa tena | Habari za Ulimwengu | DW | 09.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Kambi ya jeshi la Ujerumani yashambuliwa tena

Wanajeshi wa Ujerumani wameshambuliwa kwa mara nyingine tena huko nchini Afghanistan.

Msemaji wa wizara ya ulinzi mjini Berlin amesema kuwa kambi ya wanajeshi wa Ujerumani Bundeswehr iliyo katika mji wa kaskazini wa Kundus imeshambuliwa kwa makombora manne.

Hakuna taarifa zozote za majeruhi au vifo kufuatia shambulio hilo.

Siku mbili zilizopita kambi hiyo ya wanajeshi wa Ujerumani ilishambuliwa na askari watatu wakajeruhiwa.

Wakati huo huo muhandisi wa Kijerumani anaeshikiliwa na kundi la Taliban ametowa mwito kwa serikali za Ujerumani na Afghanistan kusaidia ili aachiliwe na watekaji nyara wanaomzuilia.

Muhandisi huyo bwana Rudolph Blechschmidt ameeleza kwamba hivi majuzi alikabidhiwa kwa watumishi wa shirika la msalaba mwekundu kwa muda mfupi na kuchukuliwa tena na kundi la Taliban.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com