Kabul. Ujerumani yatakiwa kusimama imara. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul. Ujerumani yatakiwa kusimama imara.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai, ameitaka Ujerumani kuendelea kuwa imara kuhusiana na tukio la Wajerumani wawili ambao wanashikiliwa mateka nchini Iraq.

Karzai alikuwa akizungumza katika mahojiano na televisheni ya taifa ya Ujerumani.

Wateka nyara wamesema kuwa watawauwa mateka wao mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 61 na mtoto wake wa kiume iwapo Ujerumani haitaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan ifikapo Jumanne.

Ujerumani ina wanajeshi 3,000 nchini Afghanistan kama sehemu ya majeshi ya usaidizi wa kimataifa wa usalama yanayoongozwa na NATO. Karzai atafanya mazungumzo na kansela Angela Merkel mjini Berlin leo Jumatatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com