Migogoro
Nchi za Kiarabu kujadili mashambulizi ya Iran Jumapili
7 Machi 2026
Matangazo
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya hiyo Hossam Zaki amekiambia kituo cha televisheni cha al-Qahera kuwa mkutano huo utafanyika kwa njia ya video. Nayo tovuti ya habari ya taifa nchini Misri al-Ahram imeripoti kuwa mkutano huo umeitishwa kutokana na ombi lililotolewa na Saudi Arabia.
Mashambulizi ya kulipiza kisasi yaendelea kushuhudiwa Ghuba
Iran imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika baaadhi ya nchi za Mashariki ya Kati tangu Marekani na Israel zilipofanya mashambulizi ndani ya ardhi yake. Mashambulizi ya Iran yamekuwa yakizilenga kambi za kijeshi za Marekani na sehemu nyingine zikiwemo viwanja vya ndege.