Juhudi za kuwasaka waasisi walioteka mabomu ndani ya magari mjini London zimeshika kasi | Habari za Ulimwengu | DW | 30.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Juhudi za kuwasaka waasisi walioteka mabomu ndani ya magari mjini London zimeshika kasi

London:

Juhudi za kuwasaka waasisi wa njama iliyoshindwa ya mashambulio ya mabomu mjini London zimeshika kasi nchini Uengereza.Polisi imesambaza picha kadhaa za watuhumiwa zilizonaswa na kamera katika eneo mashuhuri la Piccadilly Circus mjini London.Wawakilishi wa idara za usalama na mawaziri wa serikali ya waziri mkuu mpya Gordon Brown wamepangiwa kukutana hii leo kuzungumzia hatua zaidi zinazobidi kuchukuliwa.Jana polisi waliyategua mabomu mawili yaliyofichwa ndani ya magari mjini London-mabomu ambayo yangeripuka yangeweza kugharimu maisha ya mamia ya watu.Maafisa wa usalama wanaamini magaidi wa al Qaida wako nyuma ya njama hizo.

Hofu zimezidi nchini Uengereza ambako wananchi wanaadhimisha miaka miwili tangu mashambulio ya mabomu ya mjini London yaliyogharimu maisha ya watu 52.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com