Jeshi la Iran lakanusha kuwepo kwa mazungumzo na Marekani
25 Machi 2026
Matangazo
Jeshi hilo la Iran linasema Marekani iko katika mazungumzo peke yake.
Hatua hiyo ya Kamandi ya Pamoja ya Jeshi la Iran inayodhibitiwa na wakuu wenye misimamo mikali kutoka Jeshi la Mapinduzi kukanusha kuwepo kwa mazungumzo, inakuja wakati ambapo ripoti zinaarifu kuwa Marekani imetoa mpango wa hoja 15 za kujadiliwa katika mazungumzo hayo kwa Tehran.
Uongozi wa Iran awali ulisema kuwa hauwezi kuingia katika majadiliano na Marekani kwa kuwa nchi hiyo iliishambulia mara mbili wakiwa kwenye mazungumzo.
Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi yaliyolenga miundo mbinu kote mjini Tehran.
Kuwait na Saudi Arabia nazo zimesema zimezuia mashambulizi ya droni ingawa hazikutaja zilikotokea droni hizo.