JAKARTA: Idadi ya wahanga wa tetemeko la ardhi yaongezeka | Habari za Ulimwengu | DW | 16.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Idadi ya wahanga wa tetemeko la ardhi yaongezeka

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika mitetemeko mikubwa ya ardhi nchini Indonesia, imefikia 23.Vile vile kama watu 90 wengine walijeruhiwa,huku waokozi wakiendelea kusaka watu chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka. Inahofiwa kuwa watu wengi bado wamenasa chini ya ya nyumba zilizoteketezwa na mitetemeko hiyo. Zaidi ya nyumba 13,000 ama zimebomoka au zimeteketezwa kabisa.Shule,misikiti na hospitali ni miongoni mwa majengo hayo.Maelfu ya watu hawana mahala pa kukaa na wengine wanaogopa kurejea ndani ya nyumba zao.Ndege za uchukuzi zinajaribu kudondosha misaada kwa wakazi walionasa katika visiwa vilivyo nje ya mwambao wa Sumatra.Visiwa hivyo vilikumbwa na tetemeko la ardhi na gharika dogo la Tsunami.Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea siku ya Jumatano nje ya pwani ya Sumatra lilifuatilizwa na mkururo wa mitetemeko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com