1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Israel yasema wanamgambo wa Hamas lazima wapokonywe silaha

11 Desemba 2025

Israel imesema Hamas lazima ipokonywe silaha, baada ya pendekezo la kiongozi wa kundi hilo, Khaled Meshaal, la kutaka kuzuwia silaha hizo badala ya kuzitoa kabisa.

https://p.dw.com/p/55B8j
Israel Jerusalem 2025 | Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Abir Sultan/Pool/AFP/Getty Images

Hamas inatakiwa kupokonywa silaha zake zote kama ambavyo mpango wa amani unaoungwa mkono na Marekani unavyoagiza.

Mpango huo unatokana na makubaliano ya usitishaji vita tangu Oktoba 10, 2023, lakini hali bado ni tete, huku pande zote zikilaumiana kwa uvunjaji wa makubaliano hayo.

Afisa wa Israel ameiambia AFP kuwa  chini ya "mpango wa vipengele 20,” Hamas haitakuwa na jukumu lolote Gaza na eneo hilo halitopaswa kuwa na shughuli zozote za jeshi.

Hatua ya pili ya mpango huo inatarajiwa kuanza hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuondoka kwa wanajeshi wa Israel na nafasi yao kuchukuliwa na kikosi cha kimataifa, huku Hamas ikitakiwa kuweka silaha chini.