ISLAMABAD:Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ajilipua karibu na makaazi ya rais | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ajilipua karibu na makaazi ya rais

Watu watano wameuwawa katika shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya kituo cha usalama cha barabarani karibu na makao ya rais Pervez Musharraf wa Pakistan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan Javed Iqbaal Cheema amesema kuwa hilo lilikuwa ni shambulio la kigaidi dhidi Eneo la makaazi ya rais la Rawalpindi linalolindwa na wanajeshi.

Watu kumi na sita wamejeruhiwa katika shambulio hilo na wako katika hali mahututi.

Eneo hilo ni karibu pia na makao makuu ya jeshi na sehemu zingine za muhimu.

Hadi sasa hakuna mtu au kundi lililothibitisha kuhusika na shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com