ISLAMABAD: Rais Musharaf anataka uchaguzi ufanyike kabla Januari 9 | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Rais Musharaf anataka uchaguzi ufanyike kabla Januari 9

Rais Pervez Musharaf ametetea uamuzi wake wa kutangaza hali ya hatari nchini Pakistan, kuahidi kujiuzulu wadhifa wake jeshini na kuapishwa kama rais mara tu mahakama kuu itakapoidhinisha kuchaguliwa kwake na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza hali ya hatari nchini Pakistan, rais Musharaf amesema uchaguzi nchini Pakistan unatakiwa ufanyike tarehe tisa mwezi Januari mwakani.

´Kwa hiyo naiwachia tume ya uchaguzi iamue tarehe maalum kulingana na mahitaji yake. Lakini nina matumaini makubwa uchaguzi utafanyika kabla tarehe 9 mwezi Januari.´

Hii ina maana kwamba siku yoyote mwishoni mwa wiki ya kwanza ya mwezi Januari uchaguzi wa bunge la kitaifa na mabunge ya mikoa utafanyika sambamba katika mikoa yote nchini Pakistan.

Rais Musharaf pia ametangaza kwamba bunge litavunjwa kuanzia Ijumaa ijayo lakini hakutaja tarehe ambapo hali ya hatari itamalizika nchini Pakistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com