1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Iran na Syria zalaani mashambulizi ya Marekani nchini Syria

26 Machi 2023

Serikali za Tehran na Damascus zimelaani vikali mashambulizi ya anga ya Marekani katika eneo la Deir Al-Zor nchini Syria

https://p.dw.com/p/4PG3G
USA - Air Force One Maschine
Picha: picture alliance/ZUMAPRESS

Mashambulizi hayo yalikuwa dhidi ya vikosi vyenye uhusiano na Iran, na yalisababisha vifo vya watu 19.

Jeshi la Marekani lashambulia nchini Syria na kuua watu 10

Washington inasema ilitekeleza mashambulizi hayo baada ya shambilio la ndege zisizo na rubani za Iran kusababisha kifo cha mkandarasi wa Marekani nchini Syria.

Wizara ya mambo ya nje ya Syria imelaani mashambulizi ya Marekani katika eneo lake, ikisema Washington imedanganya kuhusu kile kilicholengwa katika mashambulizi hayo na kwamba imevunja ahadi yake ya kusitisha vitendo vya kuyadhibiti maeneo yake.

Marekani ina takriban wanajeshi 900 katika vituo vyake kaskazini mashariki mwa Syria wanaoendelea kupambana na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS na kuunga mkono Kikosi cha Kidemokrasia cha Syria kinachoongozwa na Wakurdi, ambacho kinadhibiti sehemu kubwa ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.