IMF yaonya kuporomoka uchumi wa Marekani kutaathiri Afrika zaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

IMF yaonya kuporomoka uchumi wa Marekani kutaathiri Afrika zaidi

-

ABUJA

Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF Dominique Strauss-Kahn amesema hali ya kuporomoka kwa uchumi nchini Marekani itaathiri pakubwa ukuaji wa kiuchumi katika nchi maskini barani Afrika.Akizungumza akiwa nchini Nigeria Kahn amesema hali hiyo ya kuanza kuzorota kwa uchumi wa Marekani kutayaumiza mataifa ya Afrika ambayo yanahitaji zaidi ukuaji wa kiuchumi ambao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ulikuwa umeanza kukua.

Ametoa wito kwa nchi hizo kuanzisha sera nzuri za kiuchumi kama kuweka sehemu za akiba za mali kwa ajili ya matumizi ya uwekezaji wa muda mrefu ili kuzuia uharibifu wa kiuchumi.Amesema shirika la IMF lizima litafute njia za kuzuia nchi hizo kuingia kwenye wasiwasi wa kiuchumi pamoja na kuachana na sera ambazo zimekuwa zikisaidia katika ukuaji wa kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mkuu huyo wa shirika la IMF amesema ikiwa mzozo wa kisiasa nchini Kenya utaongezeka basi shirika hilo linaweza kufikiria ni kwa kiwango gani litaendelea na mipango yake nchini humo lakini haliwezi kufikia uamuzi wa kusimamisha mipango yake katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com